Alhamisi 7 Agosti 2025 - 22:39
Ustadh Rashad: Pendekezo la Uhuru wa Palestina kutoka kwa Mbweha Mzee na Ufaransa ni “Mchezo wa Kejeli na wa Kichekesho”

Hawza/ Ustadh Rashad amesisitiza kuwa: kutoa pendekezo la uhuru wa Palestina kutoka kwenye serikali kama ya Ufaransa ni “kejeli ya kuchekesha”! Ni jambo la kuchekesha mno kwamba serikali hii inacheza nafasi ya “polisi mwema” katika “tamthilia hii ya vichekesho” La kuchekesha zaidi ni kuungwa mkono kwa pendekezo hili na “Mbweha Mzee wa Uingereza” na “Ujerumani yenye Nasaba ya Nazi”.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, kufuatia pendekezo la “suluhisho la mataifa mawili” kwa ajili ya kutatua tatizo la Palestina, lililotolewa na Ufaransa na nguvu za Magharibi na tawala za kidikteta katika ukanda, Ustadh Ali Akbar Rashad, mwenyekiti wa Baraza la HawzaTehran Iran na Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Utamaduni na Fikra za Kiislamu, katika tamko lake amesisitiza: bila shaka pendekezo hili ni “hila hatari”, yenye nyuso nyingi, tabaka nyingi na iliyo na ugumu; hii ni mbinu mpya ya kisiasa ambayo “nguvu za Magharibi” zimeibuni kwa ajili ya “kuokoa utawala dhalimu kutoka kwenye matope ya Ghaza”, kusukuma mbele “mpango wa kifedhuli wa Mkataba wa Ibrahimu”, kushawishi tawala za kidikteta za eneo “kuihalalisha Israel”, kuutoa utawala huo kwenye upweke, na kumuwekea silaha “za kimwili” na “za kiroho” jemedari wa upinzani.

Matini ya tamko ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim

Hivi karibuni, nguvu za Magharibi kwa ajili ya kutatua suala la Palestina zimewasilisha pendekezo liitwalo suluhisho la “mataifa mawili” na “kutambua rasmi taifa la Palestina”; kwa mtazamo wa juu juu na usio na kina, huenda ikaonekana kama “pendekezo la kufungua kufuli” na tukio la kutatua tatizo; lakini je: ni fikra na nia gani iliyoko nyuma ya pendekezo hili na hatua hii? Na je, wapendekezaji wa chaguo hili ni wakweli katika kauli na vitendo vyao? Na je, “mfumo unaotawala taasisi zinazodai kuwa za kimataifa”, na kuendelea kwa uhai wa “mbwa mwitu mnyonyaji wa damu” kama utawala wa Israel, utaruhusu utekelezaji wa pendekezo hili? Na kwa kudhani uaminifu na uwezekano, je, suluhisho hili litalinda haki za kihistoria za Wapalestina zilizoporwa?

Mimi, kwa unyenyekevu, nawasilisha hoja kadhaa kuhusu “hila hii hatari” kwa taifa shujaa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, mataifa ya jemedari wa upinzani wa kimataifa, na pia dhamira zilizoamka za watu wa sehemu nyingine duniani:

Moja) Palestina ilikuwa nchi yenye historia, utamaduni na ustaarabu wa kale, ni nani walioliondoa taifa hili “kongwe” kutoka kwenye ramani ya kisiasa ya eneo, kama si nguvu za Magharibi? “Utawala bandia wa Kizayuni” umetengenezwa na kuimarishwa na serikali na mashirika gani ya kimataifa? Je, si Israel ni mtoto haramu wa “ushirikiano na njama za nguvu hizi na mashirika haya”?

Mbili) Israel mnyang’anyi na msaliti ameendelea hadi sasa na maisha yake ya aibu yaliyojaa jinai na usaliti, mauaji na uporaji kwa msaada wa fedha, silaha na ulinzi wa kijeshi na kidiplomasia kwa nguvu zipi? Kwa msingi huu tunaziambia serikali za kudanganya za Magharibi na watawala na wafalme wasaliti wa eneo: hamhitaji kuunga mkono mpango wa “kuifufua Palestina”, inatosha tu mnyooshe mikono yenu kuacha kuunga mkono utawala bandia, wapiganaji wa Palestina na jemedari wa upinzani wenyewe, kwa muda mfupi, watafufua na kuimarisha tena taifa la Palestina kwenye ramani ya dunia. Ushahidi wa ukweli huu ni kwamba: katika vita hivi vya kulazimishwa, licha ya “msaada wa pande zote” wa nguvu za Magharibi na “ushirikiano wa moja kwa moja” wa jemedari wa dunia ya ukafiri, ubeberu na udikteta, utawala bandia haukuweza kustahimili hata siku kumi na mbili mbele ya “Iran peke yake”!

Tatu) nguvu hizi ziko wapi duniani, zimeunda nchi na serikali huru ambayo sasa hii itakuwa ya pili kuhesabiwa? Kinachounda historia yao nyeusi na ya aibu si chochote isipokuwa “ukoloni” na unyonyaji, “mauaji na uporaji wa rasilimali”, “mapinduzi ya kijeshi na uvamizi”! Marekani pia ni “Zimwi” linalotikana na “mchoro wa uchawi” wa hawa hawa (kwa uvamizi wa ardhi ya kihistoria ya wenyeji wa Amerika ya Kaskazini) na 

sasa nayo yenyewe imeshindwa kudhibiti dhulma na uporaji wake!

Nne) kutoa pendekezo la uhuru wa Palestina kutoka kwenye serikali kama ya Ufaransa ni “kejeli ya kuchekesha”! Ni jambo la kuchekesha mno kwamba serikali hii inacheza nafasi ya “polisi mwema” katika “tamthilia hii ya vichekesho”! La kuchekesha zaidi ni kuungwa mkono kwa pendekezo hili na “Mbweha Mzee wa Uingereza” na “Ujerumani yenye nasaba ya Nazi”! Israel imepata mimba katika “tumbo la kukodi la Uingereza” na imekua na kulelewa katika “mapaja machafu ya baba yake haramu” Marekani!

Tano) ni nani anaweza kuamini kwamba serikali hizi na mashirika haya ya bandia yatarejesha ardhi zilizoporwa kutoka katika utawala mporaji na kuzirudisha kwa Wapalestina? Ni nani anaweza kuamini kwamba hawa wataruhusu uundwaji wa nguzo za “taifa kamili na huru” kwa watu wa eneo hili? La sivyo, “nchi” bila “ardhi”, “jeshi” na “taasisi za misingi huru”, si chochote ila “serikali ya kufikirika”

sasa nayo yenyewe imeshindwa kudhibiti dhulma na uporaji wake!
 
Sita) Je, “mfumo wa kinyama” wa sasa unaotawala taasisi za kimataifa, ambao umejengwa juu ya kanuni ya kikatili ya “haki ni ya mwenye nguvu”, na kanuni dhalimu ya “haki ya kura ya turufu (veto)” inayotolewa kwa mataifa yenye nguvu ili kufuta uamuzi wowote usiokubaliana na matakwa yao, utaruhusu kutekelezwa kwa haki za wamiliki halisi wa ardhi ya Palestina na kuundwa kwa taifa huru? Je, nguvu za Magharibi na Kiarabu zinaweza kuvuka “mstari mwekundu wa irada ya kisiasa ya Marekani”?

Saba) Bila shaka pendekezo hili ni “hila hatari”, lenye nyuso nyingi, tabaka nyingi na lenye ugumu; ni mchezo mpya wa kisiasa ambao “nguvu za Magharibi” zimeubuni ili “kuokoa utawala dhalimu kutoka kwenye matope ya Ghaza”, kuendeleza “mpango wa kifedhuli wa Mkataba wa Ibrahimu”, kushawishi tawala za kidikteta za eneo kwa ajili ya “kuihalalisha Israel”, kuutoa utawala huo kutoka kwenye upweke, na kumuwekea silaha “za kimwili” na “za kiroho” jemedari wa upinzani.

Matokeo ya pendekezo na hatua hii (kama tukifaradhisha kuthibiti), yatakuwa:

“kuondoa muqawama”, “utawala wa bila kikomo” mtiririko wa wapatanishi na waliowasaliti “shirika linalodaiwa kuwa la ukombozi” na mamlaka ya kujitawala juu ya hatima ya taifa la Palestina lenye kudhulumiwa, kuanzishwa kwa “gereza kubwa la wazi” kwa ajili ya Wapalestina, na kuundwa kwa “uwanja rahisi wa kuwinda” kwa ajili ya kuliwinda mara kwa mara taifa hili lisilo na ulinzi na silaha, na kwa mkono wa utawala wa uvamizi.

Nane) Ikiwa wanaodai ni wakweli, basi wakubali na kutekeleza “pendekezo la kidemokrasia” na lenye maendeleo la kiongozi mwenye upeo wa mbali na mwenye nia njema kwa umma wa Kiislamu, kiongozi mwenye busara wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah al-Udhma Khamenei (Mola amuhifadhi) [linalojikita juu ya kura ya maoni kutoka kwa wamiliki halisi na wa kihistoria wa Palestina].

Neno la mwisho ni kwamba: Uhuru na kujitegemea kwa Palestina na kutekelezwa kwa haki za Wapalestina, havitapatikana isipokuwa kupitia:

1. “Kuendeleza na kupanua muqawama wa kivita” na jihad ya kijeshi yenye imani na ujasiri;

2. “Kupigwa kura ya maoni kwa ushiriki wa wamiliki halisi na wa kihistoria wa ardhi ya Palestina”.

Njia ya pili pia inategemea kufanikisha kwa kiwango kikubwa na cha wazi jihad ya kijeshi yenye ushujaa na ikhlasi.

Wasalamu alaykum.

Ali Akbar Rashad
Mordad 1404

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha